Cha Kutumaini Sina, Ila damu yake Bwana,
- Cha kutumaini sina, Ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha, Dhambi zangu kuziosha,
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye Mwamba: ni salama
Ndiye Mwamba: ni salama
- Njia yangu iwe ndefu, Yeye hunipa wokovu,
Mawimbi yakinipiga, Nguvu zake ndiyo nanga.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye Mwamba: ni salama
Ndiye Mwamba: ni salama
- Damu yake na sadaka, Nategemea daima,
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye Mwamba: ni salama
Ndiye Mwamba: ni salama
- Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani,
Nikivikwa haki yake, Sina hofu mbele zake.
Kwake Yesu nasimama,
Ndiye Mwamba: ni salama
Ndiye Mwamba: ni salama
Maoni ya karibuni