Matokeo Kidato Cha Sita 2017 Yametolewa Rasmi


16 July 2017 Facebook Twitter LinkedIn Google+ Matokeo,Matokeo 2017,Mtokeo Kidato cha Sita 2017


Matokeo kidato cha sita Feza GirlsMatokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2017 ulofanyika mwezi Mei mwaka huu yametangazwa jana Jumamosi, Julai 15,2017 huku shule ya Wasichana ya Feza Girls ikiendelea kufanya vizuri kwa watahiniwa wake wote 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili tu.  Shule nyingine zilizofanya  vizuri ni  Marian Boys, iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri  ya Arusha, nafasi ya tatu.

Kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 1.33 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2015. 

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari katibu mtendaji wa NECTA Bw. Charles Msonde amesema kuwa licha ya ufaulu kushuka, kiwango cha ubora wa watahiniwa katika madaraja ya ufaulu imeongezeka, ambapo kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2016 ni asilimia 97.32 ikilinganmishwa na asilimia 98.65 mwaka 2015.  Bw. Msonde ameendela kusema kuwa kati ya watahiniwa 74,896 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita watahiniwa 956 hawakufanya mtihani kwa sababu mbalimbali, wavulana waliofaulu ni 39,466 sawa na asilimia 97.55 na wasichana waliofaulu ni 24,062 sawa na asilimia 98.59.

Shule 7 kutoka Unguja ni miongoni mwa zilizoshika mkia ikiwemo Azania ya jijini Dar es salaam.
Shule 10 za mwisho Mpendae, Ben bella ,Tumekuja,Green Bird Boys, Jang’ombe, Kiembesamaki, Tanzania Adventist, Ala_ihsan girl, Azania na Lumumba .

Zilizoongoza ni Kisimiri, Feza Boys, Alliance Girls, Feza Girls, Tabora Boys, Marian Boys, Kibaha, Mzumbe, Ilboru na Tandahimba.

Bonyeza hapa kuona Shule za Sekondari 10 Bora Matokeo Kidato cha Sita 2017

Bonyeza hapa kuona Shule za Sekondari 10 Zilizoshika mkia Matokeo Kidato cha Sita 2017

 

Comments
Translate »
%d bloggers like this: